Wanaume watakiwa kutoa taarifa za ukatili wa majumbani

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Iringa, ASP Elizabeth Swai, amewasihi wanaume kuacha tabia ya kuvumilia kimya kimya vitendo vya ukatili vinavyotokea ndani ya ndoa zao na badala yake watoe taarifa kwa mamlaka husika ili kudhibiti migogoro ya kifamilia.

Akizungumza Novemba 23 mwaka huu katika kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanaume Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Swai amesema kukaa kimya kunachochea migogoro zaidi ambayo huathiri pia watoto na jamii kwa ujumla.

Alihimiza pia wanandoa kushirikiana katika malezi bora ya watoto na kuwataka kufuata utaratibu wa kisheria endapo itatokea sababu ya kuachana, ili kuepusha matatizo yanayoweza kuzuilika.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii