Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ameahidi kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya Wizara yake na Mkoa wa Morogoro katika kuendeleza juhudi za uhifadhi na kuongeza thamani ya rasilimali za maliasili na utalii mkoani humo.
Ametoa kauli hiyo leo, Novemba 24 mwaka huu alipowasili mkoani Morogoro na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Adam Malima, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika baadhi ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa Wizara itaendelea kushughulikia kwa haraka changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwemo ulipaji wa kifuta jasho na kifuta machozi kwa wale walioathiriwa na wanyamapori, kwa kutambua thamani na utu wa wananchi.
Waziri Dkt. Kijaji ameambatana katika ziara hiyo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb).
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime