Mwanafunzi Mwenye Umri Wa Miaka 19 Kumpachika Mimba Mwalimu Wake.

Richard Nana Sam, mwanamume mmoja kutoka Ghana ambaye alihuzunishwa na matukio ya hivi majuzi yaliyotokea nyumbani kwake aliamua kuyasimula kwenye mitandaoni kwa matumaini ya kupata suluhu.
Akisimulia masaibu hayo katika kundi maarufu la Facebook la Tell It All la Ghana, Richard alifichua kwamba aliamua kuajiri mwalimu wa nyumbani kwa pacha wake (mvulana na msichana) ambao wote wana umri wa miaka 19.
Alisema hakutaka kuajiri mwalimu wa kiume kwa sababu alihofia huenda akamdhuru mwanawe wa kike.
Lakini kwa mshtuko mkubwa, mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 28 alimjia siku moja na hadithi iliyoonyesha kile hasa alichokuwa akijaribu kuepukana nacho.
“Wapendwa baada ya miezi minane ya kuwasomesha watoto wangu, siku moja mwalimu wao alinijia na kuniarifu kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu wa mvulana wangu ambaye alikubali mimba hiyo ni yake," Richard alisema.
Kilichomuumiza hata zaidi ni kwamba mwalimu huyo alisema anampenda mvulana wake na kumtaka awaruhuru waoane.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii