Kampeni ya mjue jirani yake yawafikia wakazi wa Kigoma

‎Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma kupitia Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Namtumbo Oktoba 24 mwaka huu ilitoa elimu ya ki-Uhamiaji kupitia Kampeni ya Kitaifa ya "Mjue Jirani Yako" kwa Wakazi wa Kijiji cha Likusanguse Kata ya Magazini Tarafa ya Sasawala Wilayani Namtumbo.

‎‎Akizungumza katika mkutano wa hadhara na Wakazi wa Kijiji hicho kinachopakana na Nchi jirani ya Msumbiji Afisa Uhamiaji Wilaya ya Namtumbo, Mrakibu wa Uhamiaji Daudi Msuya aliwaelimisha juu ya mambo mbalimbali hususani Uraia wa Tanzaia,Walowezi na Wahamiaji Haramu katika kuhakikisha wanapata uelewa wa kutosha ili kudumisha Ulinzi na Usalama wa Nchi yetu.

‎‎Mrakibu Msuya aliwataka Viongozi na Wakazi wa Kijiji hicho kutoa taarifa kwa Idara ya Uhamiaji au kwa Vyombo vingine vya Usalama pindi wanapomtilia mashaka mtu yeyote katika makazi yao kama njia mojawapo ya kupambana na Wahamiaji haramu Nchini.

‎Mrakibu Msuya alisisitiza "Ni vyema kujenga tabia ya kutoa taarifa pindi mnapomtilia mashaka mtu yeyote katika makazi yenu hiyo ni pamoja na Viongozi kuwa na madaftari ya Wageni ili kutunza kumbukumbu ya wanaoingia na kutoka kwa kigezo cha ujirani mwema au shughuli mbalimbali hususani ni kipindi cha Mnada".

‎Aidha Mrakibu Msuya aliwataka Wakazi wa Kijiji hicho cha mpakani wasiokuwa raia wa Tanzania kujitokeza kwa wingi katika Zoezi la Utambuzi na Usajili wa Walowezi katika Mfumo wa kielektroniki ili waweze kupata haki zao stahiki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii