India na China zarejesha usafiri wa moja kwa moja wa ndege

Abiria wa safari ya kwanza ya moja kwa moja kati ya India na China katika kipindi cha miaka mitano wamewasili leo Jumatatu, baada ya mataifa hayo makubwa ya Asia kuondoa marufuku ya usafiri wa anga .

Abiria wa safari ya kwanza ya moja kwa moja kati ya India na China katika kipindi cha miaka mitano wamewasili leo Jumatatu, baada ya mataifa hayo makubwa ya Asia kuondoa marufuku ya usafiri wa anga ya muda mrefu na kufufua upya uhusiano kwa uangalifu.

Ndege ya India kutoka Kolkata ilitua katika mji wa kusini mwa China wa Guangzhou, ikiashiria kurejea rasmi kwa safari za moja kwa moja ambazo zilizitishwa tangu 2020 kutokana na janga la Uviko 19 pamoja na mizozo ya kikanda.

Mataifa hayo jirani na yenye watu wengi zaidi duniani yanasalia kuwa mahasimu wa kimkakati yanayoshindania ushawishi wa kikanda, lakini uhusiano kati yake ulidhoofika zaidi tangu mapigano makali ya mpaka wa Himalaya mnamo mwaka 2020.

Uhusiano huo unaoimarika na Beijing unakuja wakati uhusiano wa India na mshirika mkuu wa kibiashara Washington ukidorora, kufuatia nyongeza ya ushuru wa asilimia 50 wa Rais Donald Trump.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii