Baada ya Gazeti la Wall Street Journal kuripoti kuwa utawala wa Trump umeondoa kizuizi muhimu kwa Ukraine kutumia baadhi ya makombora ya masafa marefu iliyotolewa na washirika wa Magharibi, Putin alisema siku ya Alhamisi kwamba ikiwa Urusi itashambuliwa, jibu lake litakuwa ni zito sana."
Urusi imefanya kwa mafanikio majaribio ya kombora lake la nyuklia la Burevestnik, silaha yenye uwezo wa nyuklia ambayo Moscow inasema inaweza kutoboa ngao yoyote ya ulinzi, Rais Vladimir Putin amesema leo Jumapili, Oktoba 26, 2025.
Jaribio hilo pamoja na zoezi la nyuklia la wiki iliyopita, linatuma ujumbe kwamba Urusi, kwa maneno ya Putin, kamwe haitakubali shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi kuhusu vita vya Ukraine hatua inliyojiri baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuchukua msimamo mkali dhidi ya Urusi wa kuiwekea vikwazo vipya kushinikiza kusitishwa kwa mapigano.
Jenerali mkuu wa Urusi, Valery Gerasimov ambaye ni mkuu wa wafanyakazi wakuu wa vikosi vya jeshi la Urusi, amemwambia Putin kwamba kombora hilo limesafiri kilomita 14,000 (maili 8,700) na lilikuwa angani kwa takriban masaa 15 wakati lilipofanyiwa majaribio mnamo Oktoba 21 mwaka huu.
Urusi imesema ndege ya 9M730 Burevestnik (Storm Petrel) iliyopewa jina la SSC-X-9 Skyfall na NATO haiwezi kushindwa na ulinzi wa sasa na wa siku za usoni wa makombora, ikiwa na umbali usio na kikomo na njia ya ndege isiyotabirika.
Tangu kuitangaza kwa mara ya kwanza 9M730 Burevestnik mnamo 2018, Putin amefaanya silaha hizo kujibu hatua za Merika za kujenga ngao ya ulinzi wa kombora baada ya Washington kujiondoa kutoka kwenye Mkataba wa Kupambana na Balisti wa 1972 mnamo 2001, na kupanua muungano wa kijeshi wa NATO.
Putin amesema kwamba aliwahi kuambiwa na wataalamu wa Urusi kwamba silaha hiyo haiwezekani kamwe, lakini sasa, "majaribio yake muhimu" yamehitimishwa.
Huu ni ujumbe wa Putin kwa nchi za Magharibi zaidi, baada ya Marekani kuipatia Ukraine taarifa za kijasusi kuhusu malengo ya miundombinu ya nishati ya masafa marefu nchini Urusi, ni kwamba Moscow inaweza kujibu ikiwa inataka.
Baada ya Gazeti la Wall Street Journal kuripoti kuwa utawala wa Trump umeondoa kizuizi muhimu kwa Ukraine kutumia baadhi ya makombora ya masafa marefu iliyotolewa na washirika wa Magharibi, Putin alisema siku ya Alhamisi kwamba ikiwa Urusi itashambuliwa, jibu lake litakuwa ni zito sana."