LOLITA Borega aweka rekodi nyingine tena nchini Tanzania baada ya kung’ara katika mashindano ya AA Junior and Senior Open Water Swimming Championship yaliyofanyika Nyali Beach Mombasa – Kenya.
Katika hatua nyingine Borega amefanikiwa kuweka rekodi mbili muhimu – kuwa mchezaji mdogo zaidi na mwanamke wa kwanza kutoka nchini Tanzania kushiriki rasmi katika mashindano ya aina hiyo.
Hivyo alionesha uwezo mkubwa kwa kuogelea km 1.5 kwa muda wa dakika 29:54 na kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya mbio za km 3 ambako alitumia dakika 18:24 na kuipa Tanzania pointi 4 na nafasi ya saba kati ya timu tisa.
Aidha Kwa upande wa wanaume Rajab Khamisi aliogelea dakika 29:38 na Kabeer Lakhani dakika 31:47 wakimaliza kwa heshima licha ya kukosa Nusu Fainali.
Hata hivyo Meneja wa timu Ramadhan Namkoveka alisema ushiriki huo wa kihistoria umekuwa darasa muhimu kwa Tanzania kuelewa kiwango cha kimataifa.