Mvulana mwenye umri wa miaka 10-ameokolewa saa nane baada ya kukwama katika lori la takataka katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.
Mvulana huyo aliyetambuliwa na polisi kama Majed Mubarak Ibrahim, alikuwa akifaya kazi na lori linaloendeshwa na kampuni ya usafi ya taifa - Khartoum State Cleaning Corporation.
Inaaminiwa kuwa alivutwa ndani ya lori alipokuwa akitupa takataka.
Kwa sasa yuko hospitalini, lakini polisi haijatoa maelezo zaidi kuhusu hali yake.
Watu walishirikishana picha kwenye mitandao ya kijamii za wahudumu wa uokoaji wakiendelea usiku mzima kujaribu kumuokoa mvulana huyo.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema viganja vya mtoto vilikuwa vinaonekana-huku akiwa amekwama katika vifusi vya vyuma vikuu kuu.
Moja ya picha fupi ya video ya tukio hilo ilionyesha mtu mmoja akijaribu kupasua chuma, huku mwingine akihjaribu kulazimisha kufungua lori.
Umati wa watazamaji waliokuwa wakishuhudia tukio hilo ulizingira gari-huku wengine wakitoa ushauri kuhusu namna ya kumuokoa mtoto.