Methali isemayo " Umoja ni nguvu ,utengano ni udhaifu" bado inaishi katika mioyo ya watanzania ,hasa tunapomkumbuka Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kumbukizi ya miaka 26 tangu alipoondoka .
Mwalimu Nyerere alikuwa kielelezo cha busara,upendo na umoja ,mambo ambayo yalijenga msingi imara wa Taifa letu.
Mwalimu Nyerere aliamini katika nguvu ya umoja kama nguzo ya maendeleo ya taifa. Maranyingi alisisitiza kuwa watanzania hawataweza kufikia maendeleo ya kweli kama watagawanyika kwa misingi ya ukabila,udini au matabaka ya kijamii.
Alisema" Kama watanzania tutagawanyika ,hatuwezi kujenga nchi,umoja wetu ndiyo silaha yetu kubwa".
Falsafa yake ya ujamaa na kujitegemea ililenga kuimarisha mshikamano na kusaidiana kama ndugu.
Nyerere aliamini katika maadili ya utu na heshima akisema" Binadamu wote nisawa,haki ya kuishi,uhuru na heshima ni za kila mtu".
Katika kipindi hiki cha kumbukizi tunapaswa kutafakari mchango wake kwa kizazi cha sasa.
Dunia inakabiliwa na changamoto za maadili,ubinafsi na tamaa ,mambo ambayo Mwalimu Nyerere aliyaonya mapema.
Tunapomkumbuka,ni wajibu wetu kuendeleza maono yake ya umoja ,amani na upendo kwa Taifa.
Leo hii,tunaposema" Umoja ni nguvu".tunarudia maneno ambayo Nyerere, alituachia kama urithi wa kudumu .Ni wito kwa kizazi kipya kuhakikisha kuwatunalinda amani,tunathamini utu,na tunashirikiana katika ujenzi wa Taifa lenye haki na usawa.
Tukiadhimisha miaka 26 ya kumbukizi ya mwalimu Nyerere, tuombee Mungu atujalie hekima,upendo na roho ya umoja aliyoishi nayo. Tumuombe akusaidie kutenda kwa haki kuishi kwa amani na kuendelea kujenga Taifa lenye hofu ya Mungu.
" Ee Mungu wa mbinguni,tusaidie tuwe Taifa linalosimama kwa upendo na umoja.
Tujalie mioyo yenye huruma, busara na uadilifu kama kama alivyokuwa mtumishi wako Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,amani yake na urithi wake udumu milele katika vizazi vyetu".
Kumbuka ,mwalimu Nyerere si tukio la kihistoria tu,bali ni wito wa kiroho na kijamii wakuishi kwa misingi aliyotuachia.
" Umoja wetu ni nguzo ya amani,tuulinde kama tunavyolinda uhuru wetu"