Ndege ya Emirates EK9788 ilikuwa ikiwasili kutoka Dubai mwendo wa 03:50 saa za ndani ilipoacha njia na kugongana na gari la doria la uwanja wa ndege.

Ndege ya Emirates EK9788 ilikuwa ikiwasili kutoka Dubai mwendo wa 03:50 saa za ndani ilipoacha njia na kugongana na gari la doria la uwanja wa ndege.

Watu wawili wamefariki baada ya ndege ya mizigo aina ya Boeing 747 kuteleza kutoka kwenye njia ya kurukia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong na kutua baharini mapema leo Jumatatu, na kuwaua wafanyakazi wawili wa ardhini.

Ndege ya Emirates EK9788 ilikuwa ikiwasili kutoka Dubai mwendo wa 03:50 saa za ndani (19:50 GMT) ilipoacha njia na kugongana na gari la doria la uwanja wa ndege.

Watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo walifariki, huku wafanyakazi wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo wakinusurika katika ajali hiyo.

Tukio hilo limetajwa kuwa ni mojawapo ya matukio mabaya zaidi ya usafiri wa anga katika miaka ya hivi karibuni huko Hong Kong ikizingatiwa kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa jiji hilo umekuwa na rekodi nzuri ya usalama.

Mamlaka imeanzisha uchunguzi huku maswali yakisalia kuhusu njia iliyochukuliwa na ndege hiyo ilipokuwa ikitua. Maafisa wa uwanja wa ndege wamesema walitoa maelekezo sahihi kwa ndege hiyo na kwamba kuna alama kwenye njia ya kuongozea ndege.

Wafanyakazi wawili waliokufa walikuwa na umri wa miaka 30 na 41 na walikuwa na uzoefu wa miaka saba na 12 mtawalia. Ofisi ya usafiri ya Hong Kong imesema imehuzunishwana vifo vyao na kutoa rambirambi kwa familia zao.

Picha zimeonyesha ndege hiyo ilikuwa imevunjika katikati, huku sehemu ya fusela ikiwa imezama ndani ya maji huku nyufa kubwa zikionekana wazi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii