VETA yakabidhiwa vifaa vya mafunzo vyenye thamani ya Tsh, bilioni 8.4

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekabidhi rasmi vifaa vya mafunzo vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 8.4 kwa vyuo 63 vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Oktoba 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa VETA na Wamiliki wa Viwanda, Waajiri na Wadau wa mafunzo ya Ufundi Stadi. 

Vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuboresha mazingira kufundisha na kujifunza kwa vitendo.

Vifaa hivyo vimenunuliwa na Serikali kwa fedha zilizotengwa katika bajeti ya Mwaka wa fedha 2024/25 kwa lengo la kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii