Putin "Hatutaki vita Ulaya tuko tayari kwa mazungumzo"

Rais Vladimir Putin amemueleza Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuwa Urusi haitaki vita barani Ulaya. Viongozi hao wawili walikutana jana mjini Moscow ikiwa ni juhudi za hivi karibuni za kuepusha vita. Rais Putin ameelezea utayari wa Moscow wa kufanya mazungumzo na Marekani pamoja na Jumuiya ya kujihami NATO juu ya masuala ya usalama. Kauli ya Putin imezidisha matumaini ya kupungua kwa mvutano na jirani yake Ukraine na uwezekano wa uvamizi. Lakini Rais wa Marekani Joe Biden amesema hawajathibitisha madai ya Urusi na kwamba bado kuna uwezekano wa uvamizi. Kwa upande wake Kansela Olaf Scholz amesifu hatua za Urusi za kuondoa baadhi ya wanajeshi wake akisema ni ishara inayotoa matumaini. Kabla ya mkutano wake na Putin, Scholz alikutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Jumatatu mjini Kiev.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii