Chombo kinachotarajiwa kugongana na mwezi chatambuliwa mmiliki wake

Wanaastronomia wanasema kwamba sehemu ya roketi iliotarajiwa kugongana na mwezi , mnamo mwezi Machi haikutoka kwa kampuni ya uchunguzi wa anga ya Elon Musk kama ilivyodhaniwa.

Badala yake wanaamini ni roketi ya China iliorushwa angani 2014. Athari za kugongana huko hazitakuwa kubwa , wanasayansi wamesema.

Wanaanstonomia mara ya kwanza walitambua mashine ndogo iliokuwa ikielekea kugongana na Mwezi tarehe nne mwezi Machi mnamo mwezi Januari.

Machine iliorushwa angani na ambayo imekataa kurudi duniani baada ya kukamilisha ujumbe wake huitwa Space Junk.

Mchanganuzi wa data Bill Gray alitambua kifaa hichokuwa falcon 9 Booster kilichorushwa angani na bilionea Elon Musk katika mpango wake wa Spaxe X.

Lengo la Bwana Musk ni kutaka binadamu kwenda kuishi katika sayari nyingine.

Lakini sasa Bwana Gray anasema kwamba alifanya makosa na badala yake ana imani ni roketi iliorushwa angani mwezi Oktoba 2014 ukiwa ni ujumbe wa China wa Change 5-T1 uliorusha na chombo  hicho angani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii