Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Mbinga limeazimia
kumfukuza kazi mfanyakazi mmoja wa halmashauri hiyo kwa kosa la utoro
kazini huku likiwapeleka kwenye kamati ya maadili wafanyakazi watatu wa
halmashauri hiyo wakiwa na makosa hayo hayo ya utoro katika vituo vyao
vya kazi.
Akisoma maamuzi ya baraza hilo Desdeurius Haule, ambaye ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema baraza limeazimia kumfukuza kazi mfanyakazi mmoja pia limewapeleka katika kamati ya maadili wafanyakazi watatu wa halmashauri hiyo kwa makosa hayo hayo ya utoro katika vituo vyao vya kazi.