Wanasayansi wanaendelea kutafiti kisayansi kuhusu njia
mpya ya uzazi itakayotumika kutengeneza mtoto maabara bila kufuata njia
za kawaida za uzazi zinazohusisha ubebaji wa mimba na kuzaa.
Njia hii inaenda mbali zaidi, kuliko inayotumika sasa, ambayo mwanamke anaweza kupandikizwa mbegu na kuzaa bila kujamiiana.
Wanasayansi
hao wanachokifanya sasa ni kutengeneza mfuko wa uzazi wa binadamu nje
ya tumbo lake lengo ni kufanya mfumo huweze kubeba na kutunza mtoto sawa
na mfumo wa mwanadamu.
Majaribio ya utafiti huo yamefanyika kwa kutumia kondoo na kufanikiwa.