Umoja wa Mataifa kukamilisha ripoti kuhusu athari za ongezeko la joto

Wanasayansi na maafisa wa serikali wanakutana leo kukamilisha ripoti muhimu ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ongezeko la joto duniani linavyoyavuruga maisha ya watu, mazingira yao ya asili na sayari yenyewe ya dunia. Jopo la kiserikali la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mabadiliko ya tabia nchi, IPCC, linalowaleta pamoja mamia ya wanasayansi wabobezi duniani kote, hutoa ripoti tatu kubwa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kila baada ya miaka mitano au saba. Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo, Debra Roberts, ambaye ni mwanasayansi wa mazingira kutoka Afrika Kusini amesema wana wasiwasi kwamba hali ya tabia nchi inabadilika na watu wanataka kufahamu hii ina maana gani katika maisha yao ya kila siku, ndoto zao, ajira, familia na makazi yao. Ripoti hiyo inatarajiwa kukamishwa mwishoni mwa mwezi huu wa Februari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii