Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Nchi ya Umoja wa Falme
za Kiarabu (UAE) Mhe.Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan tarehe 13
Februari, 2022 ametembelea Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo
2020 Dubai na kupokelewa na Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Nchi za Falme
za Kiarabu (UAE) Mhe.Balozi Mohamed Abdullah Mtonga ambaye pia ni
Kamishna Jenerali wa Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020
Dubai.
Mara alipowasili kwenye Banda la Tanzania, Mheshimiwa
Balozi alitumia fursa hiyo kumshukuru Mgeni wake Mhe. Zayed kwa kuchagua
kuitambelea Tanzania miongoni mwa nchi washiriki 192. Aidha,
aliishukuru Serikali ya UAE kwa kuandaa vizuri Maonesho makubwa ya Expo
2020 Dubai Pamoja na uwepo wa changamoto ya kuenea kwa ugonjwa wa COVID
-19. Katika Maonesho haya Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 ambapo kwa
mara ya kwanza zinashiriki kwenye mabanda la pekee yaliyojengwa kwa
ufadhili wa Serikali ya UAE
Mwisho Mhe. Zayed aliipongeza
Tanzania kwa kuwa na Banda lenye mvuto na linaloinyesha vivutio vya
utalii pamoja na fursa zilizoko katika sekta mbalimbali. Ushiriki huu wa
nchi unaoratibiwa na TanTrade unatarajiwa kuwa na matokeo yenye tija na
kuongeza idadi ya Watalii watakaoiembelea Tanzania, kupatikana kwa
wawekezaji, mitaji pamoja na masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini
Tanzania.
Tarehe 26 Februari, 2022 Tanzania itasherekea Siku ya
Kitaifa (National Day) ambapo itafuatiwa na Kongamano kubwa la Biashara
na Uwekezaji litakalofanyika tarehe 27 Februari, 2022 katika Ukumbi wa
Ballon, Hoteli ya Jumeirah Beach, Dubai. Maonesho ya Expo 2020 Dubai
yalianza rasmi tarehe 01 Oktoba, 2022 na yatafungwa rasmi tarehe 31
Machi, 2022.