Watatu wafariki kwa jiko la mkaa Simiyu

Watoto watatu wa familia tatu, wawili wakiwa wa kitongoji kimoja wamefariki kwa kukosa hewa baada ya kujifungia kwenye hema ambalo ndani yake waliweka jiko la mkaa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Annamringi Macha amewataja watoto hao kuwa ni Loveness Emmanuel Kilonzo ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tatu (9), Passion Yusuph aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la saba (14) na Mary Jackson (12).

Tukio hilo limetokea kata ya Mkula wilayani Busega mkoani Simiyu watoto hao wakiwa kwenye makambi ya Waadventista Wasabato walipowasha jiko hilo ili kupika uji. Walilalizimika kujifungia ndani ya hema lao baada ya mvua kuanza kunyesha ili kuepuka baridi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii