UBWABWA kwa wote, kilimo kwanza na nishati safi ndiyo baadhi ya ahadi zinazobeba ilani ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Katika kampeni zinazotarajiwa kuanza rasmi Agosti 28, mwaka huu chama hicho kimeweka mezani vipaumbele 10 vinavyoangazia uchumi jumuishi, ustawi wa wananchi, lishe bora, elimu bure yenye chakula shuleni na matumizi ya teknolojia kuboresha maisha ya Watanzania.
Makala hii itaangazia kwa undani ahadi na vipaumbele vitakavyobeba ilani ya Chaumma kuelekea uchaguzi mkuu ambayo ndiyo kigezo cha kupima utekelezaji wa ahadi zao wakishapata madaraka.