Naibu Rais William Ruto amewaka moto

Naibu Rais William Ruto amewaka moto baada ya Mwakilishi wa Wanawake kaunti ya Murang'a Sabina Chege kusema kwamba kiongozi huyo anafahamu vyema jinsi Jubilee iliingia mahakamani
Akizungumza wakati wa kampeni ya Azimio Kaunti ya Vihiga, Chege alimkashifu Ruto, aliyedai eti kuna njama ya kumwondoa katika kiti cha urais kumpendelea aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga.
"Mnajua kule Central nimeskia wengine wakisema tuliwaibia. Kuna ka ukweli kidogo. Lakini kama tulijua kuiba... si hata hii tutafanya ninii.. Kwani wanafikiria wao ndio wajanja? alisema.
Matamshi hayo yalionekana kumkera DP ambaye alipinga vikali kuwa yeye na Rais Uhuru Kenyatta walitumia njia zisizofaa kuhakikisha wanachukua uogozi wa taifa.
Akizungumza eneo la Naishi kaunti ya Nakuru wakati wa mkutano wa siasa wa Kenya Kwanza, Ruto alisisitiza kwamba chama cha Jubilee kiliingia madarakani kihalali.
"Sisi tulipigiwa kura na wananchi. Nataka niwaambie watu wa kuzimia wacheni propaganda na uongo. Kama hamna sera wacheni kuwachochea Wakenya na mambo ya wizi wa kura," kiongozi huyo alisema.
Aliwasuta wanasiasa wa mrengo wa Azimio la Umoja unaoongozwa na Kinara wa Kenya kwa kupanga njama ya kuwapiganisha wananchi, jambo ambalo alisema yeye na kikosi chake hawataruhusu lifanyike.
"Washindani wetu sasa wamekubali kuwa tumewashinda kwa ajenda na kura... Sasa wameamua kugeukia siasa za kuvuruga uchaguzi. Tunataka kuwaambia tuko tayari kukabiliana nao. Tuna Mungu na Wakenya wako upande wetu," Alisema DP Ruto.
Kwa upande wake, kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi alisema mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi ulioibiwa ni ya kutowajibika na hayafai kuvumiliwa katika nafasi ya kidemokrasia."Uliona mmoja wa maajenti wa mradi wa Azimio kule Vihiga jana akisema ajenda yao ni kuiba kura.
 Hatuwezi tukakubali uchaguzi kuibiwa. Kama mumekuwa mkieneza ujumbe wa amani na kuunganisha Wakenya, nyinyi wanaazimio hanmfai kuzungumza kuhusu kuiba kura," Mudavadi alisema.Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua alisema UDA imejitayarisha vilivyo kwa uchaguzi ujao, akibainisha kuwa watapeleka angalau mawakala saba katika vituo vyote vya kupigia kura kulinda kura zao.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii