Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda yanakosoa sheria inayopendekezwa ambayo itawaadhibu watu wanaokataa chanjo wakati wa mlipuko wa maradhi wa hadi miezi sita jela.
Wiki iliyopita, waziri wa serikali wa Uganda anayehusika na biashara alipendekeza marekebisho ya Sheria ya Afya ya Umma ambayo itafini a faini na vifungo vya jela kwa wale wanaokwepa hatua zilizokusudiwa kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.
Muswada huo hautaji COVID-19 haswa, lakini bila shaka, COVID-19 ndio ugonjwa ambao nchi na ulimwengu unashughulika nao hivi sasa. Mswada huo unasema kwamba yeyote anayeficha ugonjwa wa kuambukiza anaweza kukabiliwa na faini ya $850 au kifungo cha hadi mwaka mmoja jela.
Wasimamizi wa shule wanaopokea wanafunzi bila ushahidi wa chanjo, au mzazi ambaye atashindwa kuwasilisha mtoto wake kwa ajili ya chanjo, anaweza kufungwa jela hadi miezi sita, faini ya takriban $1,100 au zote mbili.