Utawala wa Burkina Faso wafuta tume ya uchaguzi

Utawala wa kijeshi wa Burkina Faso chini ya Kapteni Ibrahim Traoré umevunjalia mbali tume ya uchaguzi nchini humo ukiitaja kuwa ni ufujaji wa fedha na Badala yake wizara ya mambo ya ndani itashughulikia uchaguzi katika siku zijazo

Tangu utawala huo ulipoingia madarakani Septemba 2022, viongozi wake mapinduzi wameanzisha mageuzi makubwa, ikiwa ni pamoja na kuahirishwa kwa uchaguzi ambao ungesababisha kurejea kwa utawala wa kiraia.

Uchaguzi mkuu ilitarajiwa kufanyika mwaka jana, lakini serikali ya kijeshi iliongeza muda wa mpito kwa demokrasia hadi Julai 2029, na kumruhusu kiongozi Kapteni Ibrahim Traoré kusalia madarakani na kuwa huru kugombea uchaguzi ujao wa urais.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii