Mbulu zaidi ya wananchi laki 1 wanufaika na mradi wa maji safi

Mradi wa wa tenki la maji Dambia  uliopo kata ya Bashay, Kijiji cha harsha Mkoani Manyara, wenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita laki mbili ulioghalimu zaidi ya bilion 41 umezinduliwa rasmi hii leo na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru unao endelea kumulika miradi mbali mbali katika wilaya ya Halmashauri ya mji Mbulu,

Akisoma risala hiyo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw. Onesmo Mwakasege amasema mradi huo unatarajia kuhudumia zaid ya vijiji ishirini na moja kwani mradi huo unauwezo wa kuzalisha maji ya kutosha kutokana na chemba zenye kasi kubwa ya uzalishaji,

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bw. Ismail aly ussi amewapongeza Ruwasa mkoa wa Manyara kwa kusimamia vyema mradi huo huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia  Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kumtua ndoo mama kichwani,

Kwa upande wa wananchi wana wanaoishi katika kata bashay kijiji cha harsha wameshukuru uwepo wa mradi huo kwani utatatua changamoto ya maji kwao.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii