Chaumma watwaa ofisi ya Chadema wilayani Same

Katika tukio la kushangaza na kuzua gumzo mapema leo, viongozi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) wamechukua rasmi ofisi iliyokuwa inamilikiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

Hatua hiyo imesimamiwa na Mwenyekiti wa CHAUMMA Mkoa wa Kilimanjaro, Gervas Mgonja, akishirikiana na Katibu wake wa Mkoa Basil Lema, ambapo viongozi hao waliwasili asubuhi katika jengo hilo kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kukabidhiwa rasmi.

Akizungumza kwa njia ya simu, Gervas Mgonja amefafanua kuwa ofisi hiyo kwa miaka zaidi ya 12 ilikuwa chini ya usimamizi wake wakati akiwa mwanachama wa CHADEMA, kabla ya kuhamia CHAUMMA.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii