Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo wanatarajiwa kusaini mkataba muhimu mjini Washington wa kumaliza mzozo uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la mashariki mwa Kongo ambapo mzozo huo umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kusababisha mateso makubwa kwa raia wa kawaida katika maeneo yaliyoathirika.
Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa mstari wa mbele katika kusukuma juhudi za kidiplomasia ambazo hatimaye zimezaa matunda kwa kufikiwa kwa mkataba huu na uongozi wake umetoa nafasi kwa mazungumzo ya kina kati ya pande husika, huku akihakikisha kwamba Marekani inatoa msaada wa kutosha kuleta suluhisho la kudumu.
Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Tommy Pigolt, mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na Kongo wameshawasili Washington tayari kwa hafla ya kusaini vilevile kkataba huo utatiwa saini mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio katika hafla maalum inayolenga kuonyesha mshikamano na dhamira ya kweli ya amani.
Aidha katika taarifa ya pamoja iliyotolewa kabla ya hafla hiyo, Mataifa hayo matatu yamesisitiza kuwa mkataba huo utaheshimu mipaka ya kimataifa utapiga marufuku machafuko ya aina yoyote na utaweka utaratibu wa kupokonya silaha makundi yote yasiyo ya kiserikali yaliyojihami huku lengo kuu ni kurejesha utulivu wa kudumu na amani kwa wakazi wa mashariki mwa Kongo.