TRC kuongeza safari za treni kutoka Dodoma-Dar

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuongeza safari za treni kati ya Dodoma na Dar es Salaam kwa tarehe 27 na 28 Juni 2025. Safari hizo zimeongezwa ili kukidhi mahitaji ya usafiri kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaorejea kutoka Dodoma, hasa baada ya kuhitimishwa kwa shughuli za Bunge.

Kwa mujibu wa ratiba, treni ya kwanza itaondoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam tarehe 27 Juni 2025 saa 1:20 usiku, na treni ya pili itaondoka tarehe 28 Juni 2025 saa 12:50 asubuhi.

TRC inawasisitiza abiria kufika stesheni angalau saa mbili kabla ya muda wa kuondoka, na kununua tiketi kupitia tovuti sgrticket.trc.co.tz ili kuepuka usumbufu

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii