Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu leo Juni 27,2025 amefika katika Mahakama ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya kesi yake dhidi ya Jamhuri.
Lissu amefungua kesi hiyo namba 14496/2025 akiomba marejeo ya mahakama kuhusu uamuzi uliotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi yake ya uchochezi ambayo ilikubaliana na maombi ya Jamhuri kusikiliza mashahidi wa siri.
Katika maombi hayo Lissu anadai kutowafahamu mashahidi hao wa siri na kuna athiri haki yake ya kujitetea ipasavyo na inaweza kupelekea maamuzi yenye athari kubwa kwake binafsi.