NATO yakubali kuongeza Bajeti ya Ulinzi hadi asilimia tano

KATIBU Mkuu mpya wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark Rutte, amesema hatua ya kuongeza bajeti ya ulinzi hadi asilimia tano ya pato la Taifa ni uamuzi mkubwa na muhimu kwa usalama wa mataifa wanachama.

Rutte alitoa kauli hiyo jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini The Hague, akibainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha uwezo wa kijeshi wa NATO ifikapo mwaka 2035.

Amesema mpango huo utaiwezesha NATO kuwa imara zaidi katika kukabiliana na vitisho vya kimataifa, hususan katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kijiusalama duniani.

Aidha, Rutte alisisitiza kuwa NATO itaendelea kuunga mkono Ukraine kijeshi, akisema ni muhimu kwa Jumuiya hiyo kuonyesha mshikamano na Ukraine dhidi ya Urusi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii