Putin hatoshiriki mkutano wa Brics

 RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, hatosafiri kwenda Brazil kushiriki mkutano wa BRICS kutokana na waranti ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Kwa mujibu wa mshauri wa masuala ya kigeni wa Ikulu ya Urusi, Yuri Ushakov, Putin atashiriki mkutano huo kwa njia ya video. Uamuzi huo umetokana na hatari ya kukamatwa endapo atasafiri katika nchi zinazotambua mamlaka ya ICC.

ICC ilitoa waranti hiyo mwaka 2023, ikimtuhumu Putin kwa kuhamisha watoto wa Ukraine hadi Urusi, baada ya uvamizi wa kijeshi dhidi ya Ukraine mwaka 2022.

Urusi imekanusha tuhuma hizo na kusisitiza haitambui ICC, ikieleza kuwa haijatia saini Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii