Wadau wa korosho wapongeza teknolojia ya uzalishaji kisasa

 WADAU mbalimbali kutoka nchi nane za Bara la Afrika zinazolima na kutumia korosho wamepongeza teknolojia ya kisasa inayotumiwa na wataalam nchini kuzalisha zao hilo (Ubebeshaji).

Hayo yamejiri wakati wa mafunzo ya siku tano yanayoendelea mkoani Mtwara kwa wadau wa korosho kutoka nchi hizo nane yenye lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo wakulima, watafiti, wabanguaji, wafanyabiashara kutoka nchi hizo ambazo ni Rwanda, Kenya, Zambia, South Sudan, Uganda, Malawi, Msumbiji na Tanzania ambayo ni mwenyeji, yanayosimamiwa na African Cashew Aliance (ACA) kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania

‘’Baada ya tunaenda kuwahimiza wakulima watumie njia hii ya ubebeshaji kwasababu mazao yatakuwa mengi zaidi, mimea itakuwa bora zaidi na ukulima kwa sasa utakuwa rahisi kuliko ilivyokuwa kabla ya kutumia njia hii,”amesema Jane.

Mshiriki kutoka nchini Tanzania, Jane Fagache amesema njia hiyo ya ubebeshaji ni bora kwasababu inaufanya mmea kukuza kwa haraka na kuleta manufaa zaidi katika uzalishaji wa korosho.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii