Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimetangaza kuwa mchakato wa kumpata mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama hicho, pamoja na kupitisha ilani ya uchaguzi, utafanyika baada ya kukamilika kwa mikutano ya awamu ya pili ya Operesheni C4C.
Kalenda ya kumpata mgombea huyo, imesogezwa mbele kwa mara ya pili mfululizo kwa sababu tofauti, awali mchakato huo ulitakiwa kufanyika Mei 10 na 11, 2025 lakini ulifunikwa kupisha tukio la kuwapokea wanachama wapya (G-55) walioihama Chadema.
Baada ya kuwapokea wanachama hao, chama kilipanga kufanikisha mchakato huo Juni 27 hadi 28 2025.
Hata hivyo tarehe hizo nazo zimesogezwa mbele kwa mujibu wa uongozi, kutokana na Kamati Kuu inayopaswa kuandaa ajenda za mkutano huo kutoketi hadi sasa.