Korea Kaskazini ilijigamba siku ya Jumanne kwamba ni mojawapo ya nchi chache tu duniani zenye uwezo wa kuweka silaha za nyuklia na makombora ya hali ya juu na ndiyo pekee iliyosimama kidete kwa "kuitikisa dunia" kwa majaribio ya makombora.
Mvutano wa kimataifa umekuwa ukiongezeka kutokana na mfululizo wa majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya balistiki ya Korea Kaskazini, hatua zilizopigwa marufuku kwa muda mrefu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Januari ulikuwa mwezi wa rekodi wa majaribio kama haya, na takribani majaribio saba, ikiwa ni pamoja na aina mpya yakombora"hypersonic" linaloweza kwenda kwa kasi.
Pia kati ya majaribio hayo ni kurusha kwa mara ya kwanza tangu 2017 kwa kombora la masafa ya kati la Hwasong-12, lenye uwezo wa kushambulia maeneo ya Marekani katika Bahari ya Pasifiki.
Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini ilisema mfululizo wa majaribio tangu mwaka mpya yanawakilisha "mafanikio ya ajabu" ambayo yaliimarisha "kuzuia vita vya Korea Kaskazini."
Pia ilinukuu Hwasong-15, kombora la masafa marefu zaidi (ICBM) kuwahi kurushwa na Korea Kaskazini, ambalo halijarushwa tangu jaribio lake la kwanza mnamo 2017, na inaaminika kuwa na uwezo wa kufika popote nchini Marekani.