Iran imetekeleza adhabu ya kuwanyonga majasusi watatu wa Israel waliokuwa wakitumikia kifungo katika Gereza la Urmia Mkoa wa Azerbaijan Magharibi nchini humo, huku Serikali ikitangaza kufanya msako na kuagiza majasusi wengine kama wapo kujisalimisha.
Utekelezaji wa adhabu hiyo umefanyika leo Jumatano Juni 25, 2025 baada ya mahakama nchini Iran kuwakuta raia hao wa Israel na hatia ya kufanya ujasusi nchini Iran ikiwemo kuingia vifaa vya kufanya mashambulizi nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Serikali la Iran (IRNA), kunyongwa kwa majasusi hao ni adhabu ya pili kutekelezwa tangu kuibuka kwa mgogoro baina ya mataifa hayo Juni 16 mwaka huu. Mgogoro kati ya Israel na Iran ulitulia jana baada ya kudumu kwa siku 13.