Mwigulu atoa utofauti wa deni la Serikali na deni la Taifa

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wananchi kutopata hofu kuhusu deni la Taifa pale linapotangazwa, kwani deni hilo lina sehemu kubwa inayoenda kwenye upande wa kampuni binafsi na wala si Serikali inayotakiwa kulipa.

Dkt. Nchemba amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha mjadala wa bajeti kuu ya Serikali ambapo amesema kuna hoja mbili ambazo wananchi wanapaswa kuzifahamu ambazo ni suala la deni la Serikali na deni la Taifa.

Amesema deni la Taifa ni deni linalohusisha deni la Serikali pamoja na deni la sekta binafsi na pale linapokuwa halina tafsiri mbaya kutokana na baadhi ya kampuni binafsi

hukopa kutokana na kutokuwa na mitaji ambapo mkopo huo huingizwa kwenye deni la Taifa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi hawahitaji kushtuka kuhusu habari ya deni la Taifa kwa sababu ya sehemu kubwa inaenda kwenye upande wa makampuni binafsi na wala si Serikali inayotakiwa kulipa.

Aidha, amesema kwa upande wa deni la Serikali ni deni linaloangaliwa kwa kuhusianisha na mapato ya Serikali ambapo Serikali hutumia utaratibu wa kukopa ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ambapo kinachoitofautisha Tanzania na nchi nyingine kupewa kipaumbele cha kukopa ni nidhamu ya matumizi ya fedha hizo ambapo nchi nyingine hukosa nidhamu hiyo na kusababisha kuzuiwa kupata mikopo hiyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii