Baraza la Maaskofu lamteua Alicia Massenga kuwa Mkurugenzi hospitali ya kanda Bugando

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limemteua Dk Alicia Massenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, iliyopo jijini Mwanza.

Taarifa kwa umma iliyotolewa  Juni 23, 2025 na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Bahati Wajanga imesema Dk Alicia ataanza majukumu yake leo.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa amemteua Dk Sr. Alicia Massenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kuanzia Tarehe 23/06/2025.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Massenga amewahi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika hospitali hiyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii