Kesi ya Lissu kupangiwa tarehe nyingine tena hadi julai 15

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasis na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akizungumza na wanachama, wafuasi na viongozi mbalimbali wa chama hicho muda mfupi baada ya kesi ya Uhaini kuahirishwa.

Kesi ya hiyo ambayo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franko Kiswaga ambaye mara ya mwisho aliiahirisha baada ya Upande wa Mashtaka kuomba ahirisho ukidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP analipitia kisha atatoa taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia na kama kesi hiyo iende Mahakama Kuu ama lah,  imeahirishwa hadi Julai 15, 2025. Huku  Wakili wa Serikali Mkuu Nasoro Katuga, akiiembia mahakama kuwa shauri hilo limefikia hatua ya uamuzi wa kumshtaki ama kutomshitaki mtuhumiwa huyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii