Aliyekuwa rais wa zamani (MAT)achukua fomu ya ubunge Mbagala

Rais mstaafu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dkt Elisha Osati amechukua fomu ya kuwania uteuzi kwa ajili ya kugombea ubunge kwenye jimbo la Mbagala katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Osati ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na mbobezi  kwenye sayansi ya tiba ya mapafu pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Utafiti wa Afya za Binadamu (NatHREC) inayofanya kazi chini ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR).

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii