Askofu Emmaus Mwamakula ameongoza maombi ndani ya chumba cha mahakama kabla ya kuanza kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu leo Julai 1, 2025.
Ambapo ulinzi uliimarishwa Kisutu wakati Lissu akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza kesi zake mbili.
Aidha ulinzi huo umeanzia katika lango la kuingilia katika Mahakama hiyo hadi katika ukumbi namba moja ambapo kesi hizo mbili zitasikilizwa hapo.
Hata hivyo Lissu amefikishwa mahakamani hapo saa 2:45 asubuhi na kupelekwa mahabusu iliyopo katika Mahakama hihiyo
Na hivi leo Julai Mosi, kesi zake mbili zitatajwa katika mahakama hiyo kwa mahakimu wawili tofauti.