Kilimanjaro: Nyumba 20 Zasobwa na Maji, Mmoja Afariki

MVUA  kubwa zilizoambatana na upepo mkali zinazoendelea kunyesha baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro, zimeezua  mapaa na kubomoa nyumba  20 zilizoko katika Kijiji cha Munge  Kata ya Donyomurwak Wilaya ya Siha,na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

 

Mkuu wa Wilaya ya Siha,  Thomas Apson, amesema mvua hizo zilizoambatana na upepo ambazo zilinyesha Februari 6 na 7 mwaka huu, mbali na kuezua paa pia zimebomoa Kanisa moja na Kiwanda cha ufugaji wa Nguruwe.

Amesema baada ya nyumba hizo kuezeuliwa, zaidi ya kaya 20  hazina makazi ya kuishi na kwa sasa zinahifadhiwa na  wasamaria wema na msaada wa haraka wa haraka wa chakula na malazi unahitajika.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, ameitaka serikali ya kijiji kupitia kamati ya maafa kuwasaidia wananchi hao,  wakati kamati ya maafa ya wilaya ikifanya tathimini kujua madhara yaliyotokea katika familia hizo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii