Nyota wa Yanga ajitosa kuchukua fomu ya ubunge Iringa Mjini

MWANASOKA wa zamani wa timu ya Yanga SC, Ally Msigwa, amejitosa rasmi katika mbio za kisiasa baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Msigwa, mzaliwa na mkazi wa Manispaa ya Iringa, amesema wakati wa kuchukua fomu hiyo kuwa yupo katika siasa si kwa matamanio binafsi bali kwa nia thabiti ya kubadilisha maisha ya watu wa Iringa, hasa vijana.

Alimecheza mpira katika kiwango cha juu, nimekumbatia ndoto yangu na kuishi maisha ya kujituma. Sasa nimeamua kuwekeza uzoefu wangu katika siasa, ili kutoa dira mpya kwa vijana wa Iringa.

Ally Msigwa si jina geni kwa wapenzi wa soka. Akiwa beki wa kati wa kuaminika, aliwahi kuichezea klabu kongwe ya Yanga SC na kuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Lakini nyuma ya mafanikio hayo, Msigwa alijijengea taswira ya mchezaji mwenye maadili, anayejali jamii na mwenye ndoto kubwa nje ya dimba.

Akiwa mchezaji aliona namna ambavyo vijana wanahitaji hamasa na dira. Katika siasa nitahakikisha vijana wa Iringa wanakuwa na majukwaa ya kuibua vipaji, kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Akizungumzia chimbuko lake Msigwa alisema kuwa yeye ni mzaliwa wa Iringa Mjini hapo ndipo alikokulia, akasoma, na kuanza safari ya ndoto yake kupitia mpira wa miguu anajua kilio cha vijana, anajua changamoto za mama lishe, anajua juhudi za waalimu, wafanyabiashara na wazazi anaelewa pia fursa tulizonazo.

Msigwa anaamini kwamba taaluma ya michezo inaweza kuwa daraja muhimu kuelekea kwenye uongozi bora.

Hata hivyo uwanjani, alijifunza nidhamu, kujituma, na kufanya kazi kama timu hayo ndiyo mambo ambayo anataka kuyapeleka bungeni..

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii