Dkt, Biteko ahudhuria mkutano wa nyuklia Afrika

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amewasili Kigali nchini Rwanda, kushiriki mkutano unaohusu masuala ya nyuklia Afrika.

Mkutano huo unaoanza  Juni 30 hadi Julai 2025, unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la  kuharakisha matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.

Pamoja na ushiriki wake katika mkutano huo Dkt. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada kuhusu nishati Afrika na utashi wa kisiasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii