Maadhimisho uhuru wa Somalia kufanyika Tanzania

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa amempokea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, Abdisalam Abdi Ali ambaye amewasili nchini ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 ya Uhuru wa Somalia ambayo mgeni rasmi ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Pia, anatarajiwa kushiriki mazungumzo ya Uwili kwa ajili ya kujadili na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili na kutembelea Mbuga ya Wanyama ya Mikumi iliyopo Mkoa wa Morogoro.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii