Wakili Ajitosa Ubunge Jimbo la Mbagala

Mwanazuoni na Wakili Dk Aloys Rugazia ameibuka kwa kishindo baada ya kuchukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Mbagala, Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dk Rugazia ametimiza haki yake hiyo, baada ya taarifa ilitolewa na Katibu Mkuu wa CCM Dk Emmanuel Nchimbi ya uchukuaji fomu rasmi wa chama hicho iliyotolewa Aprili 16,2025.
Kutokana na hatua ya Dkt Rugazia kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho ni rasmi kwamba analitaka jimbo hilo na
kwamba kwa sasa anahitaji nguvu ya ziadi ya kuwashawishi wajumbe.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii