Makongo achukua fomu kuwania nafasi ya ubunge Chato Kaskazini

 Mwandishi wa habari mwandamizi wa habari za uchunguzi aliyejikita kutetea haki za binadamu, Cosmas Makongo amechukuwa fomu ya kuwania kugombea ubunge wa Jimbo la Chato Kaskazini.

Makongo aliyewahi kuwa karibu wa Hayati Dk John Pombe Magufuli amechukua fomu ya kuwania nafasi ya kugombea ubunge katika katika jimbo hilo, mkoani Geita, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza baada ya kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Chato, Makongo amesema amewiwa kugombea ubunge baada ya kufanya utafiti kwa wananchi na kubaini Chato Kaskasini inahitaji mbunge mwenye maono ya kuleta mageuzi kiuchumi, kijamii na siasa safi.

Amejitokeza kugombea uwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Chato Kaskazini kwa sababu wananchi wanahitaji msimamizi wa Ilani ya CCM mwenye maono ya kuwavusha pale walipo kwa kuwapambania ili wanufaike na fursa zinzotolewa na Serikali.

Lakini pia kuwaendeleza kiuchumi pamoja na kukuza pato la taifa kupitia raslimali zilizopo ili kulibadilisha Jimbo la Chato Kaskazini kuwa kitovu cha sekta ya utalii, uvuvi, kilimo cha kisasa,ufugaji endelevu usafirishaji wa angani, majini na nchi kavu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii