Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu hadi Julai 1, 2025 kwa ajili ya kusubiri Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupitia jalada la kesi hiyo ili kuona kama iende Mahakama Kuu au hapana.
Hatua hiyo inatokana na Upande wa Mashtaka kuomba ahirisho mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Franko Kiswaga ambapo Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alisema jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP analipitia kisha atatoa taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia na kama kesi hiyo iende Mahakama Kuu au hapana.
Baada ya kueleza hayo hakimu Kiswaga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 1, 2025 ambapo kesi hiyo iliitishwa leo kwa ajili ya kutajwa.