Mwenyekiti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ameiomba Mahakama kupewa nafasi ya kujitetee mwenyewe huku akitaja sababu ni kuwa mawakili wake kutopewa nafasi ya faragha kuzungumza naye Gerezani.
Lissu amebainisha hayo leo Jumatatu Juni 16, 2025 wakati kesi yake ikianza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jiji Dar es salaam huku hali ya ulinzi wa polisi umeimarishwa katika Mahakama hiyo
Awali katika chumba cha Mahakama, Askofu Emmaus Mwamakula alimtambulisha mmoja wa watu ambaye amesema anapaswa kuiombea kesi hiyo kabla ya kuanza
Aidha Wananchi na viongozi mbalimbali wa Chadema waliokuwepo kwenye chumba cha mahakama walisimama na wengine kufumba macho kushiriki maombi hayo
Ikumbukwe Mhe Lisu anakabiliwa na kesi mbili tofauti kesi ya uhaini pamoja na kesi kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni.