MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE UALBINO DUNIANI

Kila mwaka 13 Juni, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ualbino (International Albinism Awareness Day pia ni siku ya kutambua umuhimu wa kulinda haki za watu wenye ualbino kwa wakati huu ambapo baadhi yao wamekuwa wakiuwawa kwa imani za kishirikina pia kutambua changamoto, haki, utu na mchango wa watu wenye ualbino katika jamii.

Ikiwa kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika mkoani Kigoma na mgeni rasmi ni Waziri mkuu  Kassim Majaliwa pia jamii imetakiwa kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili  watu wenye ualbino huku wakitakiwa  kuondokana na imani potofu za kishirikina kuhusu watu hao.

Maadhimisho hayo yalianzishwa rasmi na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2014, kufuatia azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa tarehe 18 Desemba 2014. Azimio hilo lilitangaza rasmi kuwa tarehe 13 Juni kila mwaka iwe siku ya uelewa kuhusu ualbino.

Sababu kubwa ya kuwepo kwa siku hii ni kutokana na ongezeko la mashambulizi, ubaguzi, unyanyapaa na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino, hasa katika baadhi ya nchi za Afrika kama Tanzania, Malawi na Burundi. Kulikuwepo na imani potofu kuwa viungo vyao vina nguvu za kichawi, jambo lililosababisha mateso na vifo kwa wengi.

Ikiwa lengo kuu la Maadhimisho haya ni :
• Kuongeza uelewa wa jamii kuhusu ualbino na kuondoa dhana potofu.
• Kuwalinda watu wenye ualbino dhidi ya ukatili, unyanyapaa na ubaguzi.
• Kusisitiza haki sawa kwa watu wote bila kujali rangi au hali ya ngozi.
• Kutoa jukwaa la sauti yao kusikika katika jamii.
• Kusherehekea mafanikio ya watu wenye ualbino katika nyanja mbalimbali.

Aidha yapo baadhi ya Mashirika mbalimbali, serikalini na wadau binafsi wanaojitahidi kutoa misaada kwa watu hao ikiwemo:
• Miwani maalum ya macho (kwa sababu wengi wao hupata matatizo ya kuona).
• Sunscreen (krimu ya kulinda ngozi dhidi ya miale ya jua).
• Vifaa vya kujikinga na jua kama kofia pana, mwavuli, na mavazi yenye mikono mirefu.
• Elimu ya afya na sheria kwao na familia zao.
• Ufadhili wa elimu na ajira kupitia asasi zisizo za kiserikali kama Under the Same Sun na Albino Peacemakers.

Pia yapo mahitaji muhimu kwa  Watu Wenye Ualbino ikiwemo:
• Ulinzi wa maisha yao dhidi ya mashambulizi ya kimila.
• Upatikanaji wa huduma bora za afya hasa ya macho na ngozi.
• Elimu ya jamii kupinga unyanyapaa na imani za kishirikina.
• Ajira na kujumuishwa katika maendeleo ya taifa.
• Uwakilishi wa haki zao kisiasa na kijamii.

Hata hivyo   jamii  inawajubu wa kulinda kuheshimu na kuwezesha watu wote kwa usawa katika siku ya maadhimisho haya na kuwafundisha mbinu wezeshi za kulinda ngozi na sio kikwazo, bali ni uzuri wa utofauti hivyo watu wenye ualbino ni sehemu hai ya jamii yenye ndoto, matumaini na uwezo.

Ikumbukwe kuwa Mwaka ulopita  mgeni rasmi katika maadhimisho ya kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma, Tanzania, alikuwa ni Waziri wa Afya, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kauli mbiu ya  siku ya leo katika maadhimisho hayo ni   "Kushiriki katika uchaguzi ni haki kuchaguana,kuchaguliwa na kulinda haki za watu wenye Albino "

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii