MUHIMBILI YAONGEZA KITENGO KIPYA

 Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila umepongeza Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha hospitali hiyo kwa kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kuitangaza vema hospitali hiyo ndani na nje ya nchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof. Mohamed Janabi wakati wa Mkutano wa 30 Baraza la Wafanyakazi linalofanyika katika ukumbi wa PSSSF mkoani Dar es Salaam.

Prof. Janabi ameongeza kuwa kutokana na utendaji kazi wa kitengo hicho jamii imeweza kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo na kuifanya jamii kuwa na taarifa za kutosha na uhakika hivyo kuwafanya kunufaika na uwekezaji ulifanywa na Serikali yao.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii