DP Ruto Amjibu Rais Uhuru

Naibu rais William Ruto amemjibu Rais Uhuru Kenyatta baada ya kumtupia mishale ya kisiasa Jumatatu Feburuary 7
Akiongea eneo la Magharibi, Ruto amemwambia Rais kuwa hakuna kazi ambayo hufanywa afisini isipokuwa ‘theories’.
Alisema yeye huzunguka ili kutekeleza miradi na baadhi ya kazi hiyo hufanywa juu ya gari
Alisema pia amekuwa katika serikali ya Jubilee na hivyo kazi iliyofanywa pia yeye alichangia.
“Nimekuwa kwa siasa muda mrefu kabisa kujua kuwa baadhi ya kazi hupangwa afisini kama theory, na ingine hufanywa uwanjanai hata juu ya magari,” alisema Ruto
Ruto alimwambia Rais kuwa yuko tayari kwa ushindani kwenye safari ya kuingia Ikulu mwezi Agosti.
“Wanataka kuamua ni nani atarithi mamlaka, nataka niwaambie tuko tayari kwa ushindani huo. Bring it on,” Ruto alimwambia raisi uhuru hivyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii