Rais Samia afanya uteuzi wa MaDC, Makonda awekwa pembeni

Katika taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumanne Juni 24, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua Estomin Kyando kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.

Pia, Rais Samia amemteua, Ayubu Sebabile (Muheza), Thecla Mkuchika (Butiama), Angelina Lubela (Serengeti), Maulid Dotto (Mvomero), Rukia Zuberi (Mwanga), Mwinyi Ahmed Mwinyi (Arumeru) na Jubilete Lauwo (Magu) akichukua nafasi ya Joshua Nassari.

Pia, Rais Samia amemteua Mikaya Dalmia (Kigamboni), Thomas Myinga (Sikonge), Groliana Kimathi (Monduli), Upendo Wella (Tabora), Denis Masanja (Tunduru), Fadhili Nkurlu (Songwe), Salum Nyamwese (Handeni) na Frank Mkinda (Kahama).

Aidha, Rais Samia amemhamisha Solomon Itunda kutoka wilayani Songwe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Japhari Mghamba amehamishwa kutoka Wilaya ya Handeni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo huku Amir Mohamed Mkalipa akihamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza kuchukua nafasi ya Hassan Masala.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii